SPORTS WEEKEND ROUNDUP: MAN CITY MABINGWA CARABAO, MAN U NA LIVER HAKUNA MBABE, JUVE AZIDI KUJICHIMBIA KILELENI, HATTRICK YA MESSI YAMFIKISHIA MAGOLI 650, NK - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 25, 2019

SPORTS WEEKEND ROUNDUP: MAN CITY MABINGWA CARABAO, MAN U NA LIVER HAKUNA MBABE, JUVE AZIDI KUJICHIMBIA KILELENI, HATTRICK YA MESSI YAMFIKISHIA MAGOLI 650, NK1. Matokeo ya mechi za kombe la shirikisho (Azam Sports Federation Cup) yalikuwa kama ifuatavyo:


2. Klabu ya Manchester City yanyakua kwa mara nyingine kombe la CARABAO kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 120 kuisha huku matokeo yakiwa 0-0 dhidi ya klabu ya Chelsea. Moja ya jambo linalotrend hivi sasa duniani kutoka katika hii mechi ni kitendo cha kipa wa Chelsea, Kepa Arizabalaga kukataa kutolewa nje na kocha wake wakati wa penati ili aingie kipa mwingine mzuri katika kudaka penati. Kepa alimbishia kocha Maurizio Sarri huku kila mmoja akishuhudia tukio hilo na kushangaa. 


3. Mechi kali ya weekend Man United Vs Liverpool yaisha 0-0 na kuwadisappoint mashabiki wengi waliotegemea mengi kutoka katika timu zote 2. Man United ilipata majeraha ya Juan Mata, Ander Herera na Jesse Lingard katika kipindi cha kwanza tu cha mchezo huku Liverpool walilazimika kumpumzisha straika wao Roberto Firmino baada ya kujitegua enka katika kipindi cha kwanza pia. 

Mohamed Salah ameshindwa kufunga tena katika mechi dhidi ya Man United. Mbaya zaidi hakuweza hata kupiga shuti moja golini mpaka anapokuja kutolewa dakika za lala salama.


4. Lionel Messi aliteka vichwa vya habari weekend hii pia baada ya kuisaidia timu yake ya FC BARCELONA kutokea nyuma na kushinda 4-2 huku yeye akifunga magoli matatu (Hattrick) pamoja na kutoa assist ya goli la nne lililofungwa na Luis Suarez. 

Magoli hayo ya messi yaliweka rekodi tofauti. chache ni kufikisha Hattrick 50 katika maisha yake ya soka (moja nyuma ya Cristiano Ronaldo) na pia alifikisha magoli 650 katika maisha yake ya soka. What a genius!


5. Juventus wazidi kujichimbia kileleni mwa ligi kuu Italia mara baada ya kushinda mechi yao ya ugenini dhidi ya Bologna kwa ushindi wa 1-0, goli la Paulo Dybala.

6. Harry Kane arudi kwa kishindo, Tottenham wasimamishwa na kupunguzwa matumaini ya ubingwa wa ligi kuu Uingereza. Wachapwa 2-1 ugenini na Burnley huku kocha wao Mauricio Pochettino akilaumu waamuzi kwa kuruhusu mpira uliotoka nje kuingizwa ndani bila wao kuona na kusababisha goli la kwanza la Burnley. 

Mshambuliaji wao wa kutegemewa alirudi uwanjani katika meci hiyo baada ya wiki kadhaa za kuwa nje ya uwanja akiuguza maumivu aliyoyapata katika mechi dhidi ya Manchester United mapema mwezi uliopita.


7. Baada ya kuchapwa 3-1 na Simba, Azam wamtimuaa kazi kocha Hans Van Pluijm na msaidizi wake Mwambusi. Kupata matokeo mabaya ndicho chanzo kinachoongelewa kuwa sababu ya maamuzi hayo ya klabu.


8. Mbappe azidi kuwa wa moto zaidi Ligue 1. Afikisha goli 50 katika ligi hiyo na kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuweza kufikisha magoli 50 katika ligi hiyo. Atupia goli 2 Vs FC Nimes katika ushindi wa 3-0.

9. Katika NBA: Golden State Warriors wapoteza mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Houston Rockets iliyomkosa James Harden kwa 118-112; Bucks 140-128 Timberwolves, Uttah Jazz 125-109 Mavericks, Raptors 98-113 Magic, Nuggets 105-88 Clippers, Knicks 130-118 Spurs, Pelicans 128-115 Lakers, Heat 96-119 Pistons. 


10. Leicester City yamfukuza kazi kocha wao CLAUDE PUEL kutokana na matokeo mabovu ambayo timu hiyo inayapata. 

Michezo Mingine: Arsenal walishinda 2-0 dhidi ya wabishi wa St Marry, SOUTHAMPTON FC; Real madrid waishinda 2-1 dhidi ya Levante huku utata ukiwepo katika penati ya pili waliyopewa Madrid ambayo ilizaa goli la pili la Gareth Bale dakika ya 78. Atletico Madrid walishinda 2-0 dhidi ya Vilareal huku Alvaro Morata akifungua akaunti yake ya magoli kwa klabu hiyo kwa kufunga goli la kwanza. Parma 0-4 Napoli, Fiorentina 3-3 Inter Milan, Monaco 2-0 Lyon, Rennes 1-1 Marseile, Borussia Dortmund 3-2 Bayern Leverkusen, Fc Bayern Munich 1-0 Hertha Berlin, Newcastle 2-0 Huddlesfield. 

Imeandaliwa na Traves Msangule
Msanguletraves@gmail.com
+255657949023

Loading...

No comments: