Taharuki mtoto mwingine akiuawa Njombe - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 3, 2019

Taharuki mtoto mwingine akiuawa NjombeTaharuki mtoto mwingine akiuawa Njombe

Njombe. Siku mbili baada ya Jeshi la Polisi kuanza operesheni ya kuwasaka wanaofanya mauaji ya watoto wilayani Njombe, juzi saa nne usiku wananchi wa Kijiji ya Matembwe walishuhudia mwili wa Rachel Malekela ukiwa umetelekezwa kichakani.
Mbali ya tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka alisema jana kuwa watu wanne wameuawa na wananchi waliowashuku kuhusika na mauaji ya watoto katika Wilaya za Njombe na Wanging`ombe.


Pia alisema mtu mwingine mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa na wananchi katika Kijiji cha Magunguli, Mufindi mpakani na Njombe baada ya kuhisiwa kuhusika na mauaji hayo.


Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William alisema watu hao waliingia kijijini hapo Januari 31 na wananchi waliwatilia shaka licha ya kuwa watu wema. Waliwekwa chini na uangalizi wa mgambo lakini wananchi walivamia na kuanza kuwapiga hadi mmoja kufariki dunia.


Katika tukio la Matembwe, mwenyekiti wa kijiji hicho, Brayson Malekela, binti huyo aliyekuwa akisoma darasa la pili Shule ya Msingi Matembwe hakuonekana nyumbani baada ya kutoka shule.Loading...

No comments: