TAKUKURU yashikilia simu ya Zitto Kabwe kwa siku nne - Ado Shaibu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 5, 2019

TAKUKURU yashikilia simu ya Zitto Kabwe kwa siku nne - Ado ShaibuImedaiwa kuwa kwa siku nne sasa simu ya Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini bado inashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Ndugu Ado Shaibu, akiongea na Muungwana Blog amesema kuwa TAKUKURU wamesema kwamba wanaendelea na uchunguzi na bado wanaihitaji simu hiyo kwa uchunguzi.

"Simu hiyo imeshikiliwa kwa siku nne,ambapo kupitia ukurasa wa Mke wa Mh. Zitto, Anna Bwana iliripotiwa kuwa TAKUKURU waliihitaji simu hiyo kwa ajili ya uchunguzi wa madai ya Mbunge huyo kwamba baadhi ya watendaji wa serikali wamehongwa na Makampuni ya nje ili kukwamisha mradi wa uchimbaji chuma wa  Mchuchuma na Liganga," amesema Ado.

Kwa Mujibu wa Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Ado amesema kuwa simu hiyo ni ya tatu ya kushikiliwa na vyombo vya dola.
Loading...

No comments: