TETESI ZA SOKA: BAYERN MUNICH WAMESHAKUBALIANA NA TIMO WERNER, UHAMISHO KARIBUNI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 28, 2019

TETESI ZA SOKA: BAYERN MUNICH WAMESHAKUBALIANA NA TIMO WERNER, UHAMISHO KARIBUNI


Timo Werner

"Bayern Munich wanazidi kuibomoa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga" hivyo ndivyo unavyoweza kusema na sio mara ya kwanza kuusikia msemo huo kwani hawajaanza leo kuwa wanawanunua wachezaji wanaofanya vizuri kutoka timu pinzani katika ligi hiyo na kusababisha kusiwe na ushindani. 

Sasa habari za chini chini zilizovuja zinasea kuwa Straika wa klabu ya RB Leipzig, Timo Werner amekubaliana maslahi binafsi na Bayern Munich ingawa vilabu hivyo viwili bado havijakubaliana ada ya uhamisho. 


Bayern wamewahi kuwachukua wachezaji kama Leon Goretzka 2018 (Schalke 04), Serge Gnabry 2017 (Werder Bremen), Niklaus Sule 2017 (Hoffenheim), Sebastian Rudy 2017 (Hoffenheim), Manuel Neuer 2011 (Schalke 04), Benjamin Pavard 2019 (VfB Stuttgart), Robert Lewandowski 2014 (Borussia Dortmund), Mario Gotze 2013 (Borussia Dortmund), Mats Hummels 2016 (Borussia Dortmund), na wengine wengi.  

Taarifa kutoka Sports Bild nchini Ujerumani
Loading...

No comments: