TETESI ZA USAJILI: MAN CITY KUTUMIA PAUNI MIL 150 KUWAPATA WAINGEREZA HAWA WATATU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 20, 2019

TETESI ZA USAJILI: MAN CITY KUTUMIA PAUNI MIL 150 KUWAPATA WAINGEREZA HAWA WATATU


Moja ya tetesi inayosambaa sana mitandaoni leo hii ni hii ya klabu ya Manchester City kutenga kitita cha Pauni Mil.150 kwa ajili ya kuwapata wachezaji Wa kiingereza watatu ili kuimarisha kikosi chao ambacho tayari kinahesabiwa kama kikosi bora barani Ulaya.


Taarifa kutoka ndani ya klabu zinasema Majira ya kiangazi Pep Guardiola amejiandaa kutoa kiasi cha Pauni Milioni 150 ili kuwanasa wachezaji watatu wa Kiingereza ambao ni beki wa kulia wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka, beki wa kushoto wa Leicester city Ben Chilwell na kiungo wa West Ham United Declan Rice. 

No comments: