TMA:MVUA ZA MASIKA ZITAKUWA ZA WASTANI HADI JUU YA WASTANI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 14, 2019

TMA:MVUA ZA MASIKA ZITAKUWA ZA WASTANI HADI JUU YA WASTANI

MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini(TMA)leo imetoa utabiri wa hali ya hewa  kipindi cha msimu wa mvua za masika Machi had Mei 2019,Mvua zinazotarajia  kunyesha zitakuwa za wastani hadi juu ya wastani katika Maeneo mengi ya ukanda unaopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka nchini
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA,Dkt Agness Kijazi anasema  msimu huo wa mvua hizi utakuwa wa kipindi kifupi na kutarajia kuisha wiki ya kwanza ya mwezi mei.
"Wakati huo huo mvua za Msimu ambazo zilianza mwezi Novemba 2018,zinatarajiwa kuendelea hadi mwishoni mwa mwezi April 2019 ambapo mvua za Chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo machache ya kanda ya Kusini Ruvuma pamoja na mikoa ya Dodoma na Singida,"anasema  Dkt Kijazi 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agnes Kujadili akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu ya mvua za masika kipindi cha Machi -Mei mwaka huu. 
Anasema msimu wa mvua za Masika ni mahususi katika Maeneo ya Nyanda za Juu  Kaskazini -mashariki, pwani ya Kaskazini na visiwa vya Unguja na Pemba, ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma maeneo hayo yanatarajia kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani katika msimu huu wa Masika. 

"Katika baadhi ya Maeneo ya nyanda za juu kaskazini -mashariki, hususani mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kuna uwezekano mkubwa wa mvua za juu ya wastani, "anasema

Aidha anasema Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Februari katika mkoa wa Kagera na kusambaa katika mikoa ya Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga katika wiki ya pili ya mwezi machi 201,mvua zinatarajia kuwa wastani hadi juu wastani katika maeneo mengi.

"Katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba na kusambaa katika mikoa wa Tanga na Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro katika wiki ya kwanza ya mwezi Macho Ambapo mvua zinatarajia kuwa wastani hadi juu ya wastani, "anasema

Pia anasema maeneo ya mkoa wa Manyara yanatarajia kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani huku mikoa ya Dodoma,Singida,Kigoma,Tabora,Katavi,Rukwa,Mbeya,Songwe,Njombe,Iringa,Ruvuma,Lindi,Mtwara na Kusini Mwa Morogoro zinatarajiwa kuwa za wastani zinatarajiwa katika maeneo ya kati ya nchi  mikoa ya Dodoma na Singida na ya Kusini mkoa wa Ruvuma. 


Loading...

No comments: