UCHAMBUZI: JE HUU NDIO WAKATI SAHIHI WA LIVERPOOL KUIUA BAYERN MUNICH? - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 18, 2019

UCHAMBUZI: JE HUU NDIO WAKATI SAHIHI WA LIVERPOOL KUIUA BAYERN MUNICH?Na James Walker-Roberts / Traves Msangule

"MIA SAN MIA" ndio motto au kaulimbiu ya klabu ya FC BAYERN MUNICH ikimaanisha "TUPO VILE TULIVYO" au kwa lugha ya kiingereza unaweza sema "we are who we are". Swali la kujiuliza ni je, Bayern ni klabu ya namna gani hivi karibuni? 

Ni Klabu iliyoshinda kombe la ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga kwa miaka 6 mfululizo na wamefanikiwa japo kuingia nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya katika misimu 5 kati ya hiyo 6. 

Pamoja na hayo, wanapoelekea katika mpambano wao wa hatua ya mtoano dhidi ya majogoo wa Anfield, LIVERPOOL FC, wajerumani hao wanaonekana kama ni klabu ambayo ipo katika mpito na nafasi yao katika msimamo wa Bundesliga unatuambia kitu fulani. 

Wapo point 2 nyuma ya vinara wa ligi BORUSSIA DORTMUND wakiwa wamecheza mchezo mmoja zaidi yao. Katika nyakati kama hizi katika hiyo misimu 6 ya nyuma, Bayern walikuwa wanaongoza ligi wakiwa na tofauti ya point 5 dhidi ya timu inayofuatia. Na katika misimu 3 kati ya hiyo sita, muda kama huu walikuwa wanaongoza kwa tofauti ya point 19, 18 na 15 dhidi ya waliokuwa wanafuatia kwa karibu. 


Dortmund wamekuwa bora sana msimu huu wakipoteza mchezo mmoja tu mpaka sasa katika Bundesliga wakati FC Bayern wakiwa wameshapoteza michezo 4 kama walivyofanya msimu wa 2017/2018. Katika misimu miwili iliyopita walipoteza mara mbili tu. 

Pia wameruhusu kufungwa magoli 34 katika michuano yote ikiwa ni kiwango cha juu katika nyakati hizi tokea msimu wa 2010/2011. 


Ukiachana na fomu mbaya waliyonayo, Bayern pia wana watu wengi wa kuwakosa katika mechi dhidi ya Liverpool. Thomas Muller hatacheza michezo yote 2 kutokana na kadi, Arjen Robben hajacheza tangu mwezi November, Frank Ribery ndio kwanza anarudi kutoka katika majeruhi, na Tolisso ni majeruhi. Kinda Kingsley Coman, ambaye kocha Niko Kovac anasema anaipa utofauti na ubunifu Bayern, anauguza majeraha pia baada ya kuumia katika mechi aliyofunga magoli 2 katika ushindi wa 3-2 ijumaa dhidi ya Augsburg.  

Ukiacha hayo yooote tuliyozungumza, kuna hili jipya la SAFU YAO YA ULINZI. Bayern hawajapata Clean sheet tokea mwaka huu wa 2019 uanze na juzi juzi tu walipokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa timu ya Bayern Leverkusen ambao walikuwa wakicheza kwa kufanya HIGH PRESSING na spidi ya hali ya juu ikihamasisha mashambulizi ya haraka na kuleta shida sana kwa vijana wa Kovac. 

Beki wao wa kati, Mats Hummels, kiwango chake kimeshuka mno na golikipa wao namba moja Manuel Neuer hajawa katika ubora wake tokea arudi kutoka katika majeraha ya mkono. Mtandao wa WHOSCORED umeripoti kuwa Katika magolikipa 13 ambao wamecheza angalau mechi 20 za Bundesliga msimu huu, Neur ndiye mwenye asilimia ndogo/kiwango kidogo zaidi cha kuokoa michomo/mashuti yanayolenga lango lake. 

Golikipa wa Fc Bayern, Manuel Neuer

Ukiangalia mambo yote ambayo tumejaribu kuyaeleza kwenye uchambuzi huu, utagundua kuwa HUU NDIO WAKATI SAHIHI WA LIVERPOOL KUIMALIZA KABISA FC BAYERN MUNICH. 

Liverpool wapo kwenye fomu nzuri kuanzia kwenye ligi wakiwa wanaongoza na wanautafuta ubingwa, wanacheza mpira wa kasi, wanaPress kwa nguvu sana, na wana faida ya kuwa na safu nzuri ya ulinzi ikiongozwa na golikipa Allison Becker, na Virgil Van Djik huku safu yao ya ushambuliaji ikiundwa utatu mtakatifu wa Sadio Mane, Roberto Firmino na Mohamed Salah ambao wana uwezo wa kufanya makubwa na maajabu katika mechi hiyo. 


Liverpool wasindwe wenyewe kupita katika hatua hii ya mtoano.
Tchao. 
Loading...

No comments: