Uchina: Waja na mfumo wa utambuzi wa watu kwa kutambua jinsi wanavyotembea (Surveillance) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 28, 2019

Uchina: Waja na mfumo wa utambuzi wa watu kwa kutambua jinsi wanavyotembea (Surveillance)

kutambua jinsi wanavyotembea

Huko nchini Uchina kampuni moja imekuja na teknolojia ya utambuzi wa watu kwa kutambua jinsi wanavyotembea au kukaa. Teknolojia hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Gait recognition’ tayari imeanza kufanyiwa majaribio.

Uchina ni moja la taifa lenye kamera nyingi zaidi zinazotumika kwa ajili ya kutafuta na kuwatambua watu wanaohitajika na vyombo vya usalama wa nchi hiyo. Kwa sasa teknolojia inayotumika ni Facial Recognition (mfumo wa usalama wa utambuzi wa watu kwa kutambua sura zao).
kutambua jinsi wanavyotembea

Huang Yongzhen, Mkurugenzi wa Watrix, akielezea jinsi mfumo huo unavyofanya kazi.
Nchini Uchina kuna jumla ya kamera zaidi ya milioni 170 katika maeneo mbalimbali kama vile barabarani, vituo vya mabasi na treni, na sehemu mbalimbali za umma.

Je, unafahamu?

Uingereza ina jumla ya CCTV kamera milioni 5.9, na wastani wa kamera 1 kwa kila watu 11.
Teknolojia hiyo ya ‘Gait Recognition‘ imetengenezwa na kampuni inayokwenda kwa jina la Watrix, na inauweza wa kutambua watu na mienendo yao kwa umbali wa hadi mita 50. Utambuzi huu utaweza kufanyika ata kama sura zao hazionekani kwa muda huo. Tayari majiji ya Beijing na Shanghai yameshaanza kutumia mfumo huo wa usalama.
Ingawa teknolojia hii inavutia sana bado ina mapungufu kadhaa yanayotakiwa kuboreshwa:
  • Haiwezi kugundua mtu moja kwa moja, inahitaji kupewa jalada husika na utendaji kasi wake unachukua takribani dakika 10 kumtambua mtu.
  • Kwa kutumia data za uso ambazo tayari zipo, kamera zilizopo zitaweza kuongeza data za jinsi watu hao wanatembea na kukaa.
Kikubwa ni kwamba hata serikali haitaitaji kuwaomba watu kuchukua rekodi hii ya jinsi wanavyotembea wanavyoongea, n.k kwa kuwa tayari wanarekodi ya sura; kwa sasa itakuwa ni kutambua sura za mtu na kisha programu hiyo kuongezea data zao za matembezi.

Teknolojia ya Gait tayari imeshafanyiwa utafiti mwingi na mataifa mengine kama vile Marekani na Japan, ila hii ni mara ya kwanza teknolojia hiyo kutimiwa. Je, una mtazamo gani juu ya teknolojia hii?


Loading...

No comments: