UEFA CHAMPIONS LEAGUE: LEO NI ZAMU YA R.MADRID Vs AJAX, B.DORTMUND Vs SPURS - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 13, 2019

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: LEO NI ZAMU YA R.MADRID Vs AJAX, B.DORTMUND Vs SPURSRaundi ya kwanza ya hatua ya mtoano katika ligi ya mabingwa Ulaya itaendelea tena leo usiku kwa kuwakutanisha wababe wengine wa bara hilo. Real Madrid kutoka nchini Hispania itakutana na Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi huku Borussia Dortmund ya Ujerumani itakutana na Totenham Hotspurs ya Uingereza. 

Ushindi ni muhimu kwa kila timu ingawa kuna timu zina taarifa mbaya za majeruhi kama Borussia Dortmund ambao hawatakuwa na wachezaji wao Paco Alcacer, Marco Reus, Julian Weigl na Lukasz Piszczek. 

Totenham wataendelea kukosa huduma za straika wao Harry Kane, Kiungo Dele Alli, na beki wa kushoto Daniel Rose ambaye bado hakuna uhakika kama atajumuishwa katika kikosi kitakachocheza leo. 

Mabingwa watetezi Real Madrid wakiwa katika kiwango bora kabisa katika michezo ya hivi karibuni wana matumaini ya kuondoka na ushindi katika mchezo huo huku kinda Vinicius Jr akianzishwa kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Gareth Bale kwa mara nyingine. 


Nani unampa nafasi ya kushinda mechi ya kwanza ya hatua hii kati ya hizi timu? tuambie kwenye comment section hapa chini.
Loading...

No comments: