Ulimwengu aanza kung'ara Algeria - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 18, 2019

Ulimwengu aanza kung'ara Algeria


Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu jana amefungua akaunti yake ya mabao katika klabu yake mpya, JS Saoura baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 82 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Tadjenanet kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Algeria Uwanja wa Agosti 20, 1955 mjini Bechar.

Bao la pili lilifungwa na Rafik Boukbouka dakika ya 90 na ushei na kwa ushindi huo, Saoura inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi na kupanda kwa nafasi moja hadi ya sita.

Saoura watakuwa na mechi tatu zaidi za Ligi ya Algeria dhidi ya CA Bordj Bou Arreridj Februari 22 , USM Bel Abbes Februari 26 na MO Bejaia Machi 2, kabla ya kucheza mechi zake mbili za mwisho za Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika.
Loading...

No comments: