WABUNGE WAWILI CHADEMA WASAKWA


Peter LijualikaliKAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema jeshi hilo linawasaka wabunge wawili wa Chadema, Peter Lijualikali (Kilombero) na Suzan Kiwanga wa Mlimba.
Wabunge hao walikuwa miongoni mwa wanachama 13 wa Chadema walioachiwa huru na mahakama mkoani humo Januari 2019.
Waliachiwa huru kupitia kifungu cha Sheria namba 225 cha mwenendo wa makosa ya jinai baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili, ikiwa ni pamoja na kuchoma moto ofisi ya Sekondari ya kijiji cha Sofi Wilaya ya Malinyi.
Siku chache baada ya kuachiwa huru, polisi jana Jumatano Februari 20, 2019 imeeleza kuwa imewakamata wanachama saba kati ya 13.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mutafungwa alisema miongoni mwa wanachama wanaowatafuta ni wabunge wa chama hicho. Alisema hivi sasa wamejipanga kwa kuwa na ushahidi na vielelezo vya kutosha vya kuwatia hatiani.

Post a Comment

0 Comments