Wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakutana na Mkuu wa mkoa wa Kagera - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 26, 2019

Wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakutana na Mkuu wa mkoa wa Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Generali Marco Gaguti, akiongea na Wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA) ofisini kwake, mjini Bukoba tarehe 25 Feb 2019. (Picha na Thomas Salala, ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera.)

Mkuu huyo wa mkoa ameipongeza kazi nzuri ya kudhibiti na kuhimiza ubora wa maudhui ya vyombo vya utangazaji inayofanywa na Kamati ya Maudhui kwa pamoja na Sekretarieti ya TCRA.

Mhe Brig. Gen. Gaguti amewaomba Wajumbe hao kuwahimiza wanahabari katika vyombo vya utangazaji watakavyovitembelea mkoani Kagera, kuongeza juhudi katika kusukuma mbele agenda ya maendeleo mkoani mwake.

Alisisitiza, kuwa agenda ya maendeleo ndiyo itangulie mbele katika kuharakisha maendeleo ya Taifa letu.

Wajumbe wa Kamati ya Maudhui walimtembelea Mhe Brig. Gen. Gaguti kabla ya kuanza ziara ya kuvitembelea baadhi ya vituo vya utangazaji vilivyoko mkoani humo, katika kuhimiza uandaaji na urushaji wa maudhui bora ya vyombo vya utangazaji nchini, ikiwa ni pamoja na kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayoongoza sekta ya Utangazaji nchini ili kudumisha amani na kuchochea maendeleo ya sekta pamoja na Taifa kwa ujumla.

Wajumbe hao ni Valerie Msoka (Mwenyekiti), Joseph Mapunda (Makamu Mwenyekiti), Abdul Ngarawa, Jacob Tesha na Derek Murusuri.

Wajumbe hao waliambatana na ofisa wa TCRA kutoka Kanda ya Ziwa Abdul Hussein pamoja na Eunice Mabagala na Rolf Kibaja kutoka ofisi za TCRA makao makuu.

Loading...

No comments: