Waliomuibia Binti wa Raila Odinga Wafikishwa Mahakamani - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 12, 2019

Waliomuibia Binti wa Raila Odinga Wafikishwa Mahakamani


John Ayub na Christine Anyango wanadaiwa kuiba fedha kiasi cha Ksh 245,000 kwenye pochi ya Rosemary Odinga ambaye ni binti wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga

Watuhumiwa hao wanadaiwa kufahamiana na binti huyo ambapo John Ayub alikuwa mpambe wa Rosemary Odinga

Wizi huo unadaiwa kutekelezwa Novemba 15, 2018 ambapo mke wa John alishtakiwa kwa kosa la kutumia jina la mtu mwingine kusajili kadi ya simu kabla ya kuzichukua pesa hizo.
Loading...

No comments: