Wanasiasa tujifunze kidogo kuweka akiba ya maneno - Nape Nnauye - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 6, 2019

Wanasiasa tujifunze kidogo kuweka akiba ya maneno - Nape NnauyeMbunge wa Mtama kwa tiketi ya CCM,  Nape Nnauye amewataka wanasiasa akiwepo na yeye kuweka akiba ya maneno pindi wanapowashutumu wenzao.

“Wakati mwingine tunapolishwa maneno tukaseme tuweke akiba ya maneno ya nani anapinga nini na anasema nini?  Itatusaidia sana kwa sisi wanasiasa tukiweka akiba ya maneno,” amesema Nape  leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia  taarifa ya kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii..

“Tujifunze kidogo kuweka akiba ya maneno hasa tunaposhutumiana bila sababu. Wakati wa uchaguzi tulipeleka kwa Rais maombi ya kufuta baadhi ya mashamba yaliyotelekezwa,” aliongeza.

Jumatatu hii, Nape aliandika barua kwenda kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ya kujiuzulu nafasi ya uenyekiti  wa  kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
Loading...

No comments: