WASIWASI JIJINI TURIN; CRISTIANO RONALDO KUFANYIWA VIPIMO KATIKAMKIFUNDO CHA MGUU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 28, 2019

WASIWASI JIJINI TURIN; CRISTIANO RONALDO KUFANYIWA VIPIMO KATIKAMKIFUNDO CHA MGUU

cristiano

Hali ya wasiwasi imetanda katika jiji la TURIN ambapo ndipo timu ya Juventus inapotokea na ilipo kwani kuna uwezekano wa kumkosa mshambuliaji wao wa bei ghali  Cristiano Ronaldo baada ya kupata majeraha katika kifundo chake cha mguu.

Cristiano aliumia katika mechi dhidi ya Bologna ambapo Juve waliibuka na ushindi wa 1-0 ugenini huku goli likifungwa na Paulo Dybala. 

Leo klabu ya Juventus wamethibitisha kwamba Cristiano Ronaldo atafanyiwa vipimo katika kifundo chake cha mguu na majibu ya vipimo hivyo ndio yatakayoamua kuwa acheze au apumzishwe na kwa muda gani pia. 

Loading...

No comments: