WAWILI SIMBA WAANDIKA REKODI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 19, 2019

WAWILI SIMBA WAANDIKA REKODI


WASHAMBULIAJI Wa Simba, Meddie Kagere na John Bocco, Jumamosi iliyopita wamefanikiwa kuandika rekodi katika Uwanja wa Taifa baada ya kuongoza timu hiyo kuibuka na ushindi dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Ndani ya siku tano, Bocco na Kagere wamefanikiwa kuiwezesha Simba kutoka kifua mbale katika mechi mbili ilizocheza, moja ikiwa ni ya kimataifa ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly lakini pia ile ya juzi ya ligi kuu dhidi ya Yanga.

Katika mchezo dhidi ya Al Ahly Februari 12, Simba ilishinda bao 1-0, bao hilo lilifungwa na Kagere kwa shuti kali dakika ya 64 baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa Bocco. Bao hilo lilifungwa katika goli lililopo upande wa Kaskazini mwa uwanja huo.

Jumamosi iliyopita dhidi ya Yanga, Bocco na Kagere wakafanya kitu kama kile walichokifanya dhidi ya Al Ahly.

Katika mchezo huo, bao la Simba lilifungwa dakika ya 71 na Kagere kwa kichwa baada ya kupokea pasi kutoka kwa Bocco aliyopiga kwa mguu wake wa kulia.

Hata hivyo, bao hilo pia lilifungwa katika goli lilelile la upande wa Kaskazini la uwanja huo wa Taifa, likiwahusisha wachezaji walewale na kipindi kilekile cha pili


Loading...

No comments: