Wazazi wa Nandy Wampongeza Mtoto Wao kwa Kuwajengea Nyumba - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, February 2, 2019

Wazazi wa Nandy Wampongeza Mtoto Wao kwa Kuwajengea Nyumba


Wazazi wa Nandy Wampongeza Mtoto Wao kwa Kuwajengea Nyumba

Wazazi wa msanii wa Bongo, Nandy amemshukuru muimbaji huyo kwa namna alivyojitolea hadi kuwajengea nyumba.

Katika mahojiano na kipindi cha Clouds 36o cha Clouds TV wamesema Nandy angeweza kutumia fedha zake katika mambo yake binafsi lakini aliamua kujitoa kwa ajili yao.

"Tunashukuru sana kwa zawadi ya nyumba aliyotupatia kwa kweli Nandy,amekuwa
akitushirikisha sana kila akipata pesa anakuja kutuambia kuwa Mama leo nimepata million 5 au 10," ameeleza mama yake mzazi.

Ameendelea kwa kusema, 'Yeye ni kijana angeweza kufanya kitu anachokitaka kama kununua nguo, lacewig lakini kiasi anachobaki nacho ni kidogo hadi namwonea huruma,'.
Loading...

No comments: