Wazee wa 'Kamwene' Baada ya kuwagaragaza Wema na Hemedy kwenye Tuzo, washindi wafunguka - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 26, 2019

Wazee wa 'Kamwene' Baada ya kuwagaragaza Wema na Hemedy kwenye Tuzo, washindi wafunguka


Baada ya kuwagaragaza Wema na Hemedy kwenye Tuzo, washindi wafunguka
Muigizaji bora wa kike katika tuzo za  Sinema Zetu, Flora Kiyombo amesema alikuwa
akimuhofisa sana Wema Sepetu katika kinyanganyiro hicho.

Flora amefunguka hayo kwenye Mahojiano na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM ambapo
ameeleza kuwa hofu yake kwa Wema ni kutokana ana mashabiki wengi.

"Nilikiwa namuhofia Wema Sepetu sababu yeye ni msanii wa muda mrefu na amefanya filamu
nyingi na kingine anamashabiki wengi hivyo kwake ingekuwa rahisi kushinda sababu ya
umaarufu wake lakini nashukuru Mungu kwa kuweza kushinda Msanii bora wa kike," amesema Flora.

Kwa upande wake  Rashidi Kassim  ambaye ndiye mshindi wa tuzo ya msanii bora wa kiume
amesema, 'Mimi nilikuwa namuhofia Hemedy Phd kwa sababu ni msanii anayejulikana na yupo
kwenye filamu muda mrefu,'.
Loading...

No comments: