Waziri Mkuu awaonya DC na DED 'wanaorogana

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wende Ng'ahara wamalize tofauti zao na wasipojirekebisha atamshauri Rais Dkt. John Magufuli kufanya maamuzi mengine.
Waziri Mkuu awaonya DC na DED 'wanaorogana

Waziri Mkuu ametoa kalipio hilo leo Jumatano, Februari 20, 2019 wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Nyakanazi, kijiji cha Nyakanazi, Biharamuko mkoani Kagera.

Amesema kutokuelewana kwa viongozi hao ambao wakati mwingine wanatuhumiana kufanyiana vitendo vya kishirikina kumesababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo katika wilaya,

"mliletwa hapa kuiwakilisha Serikali na kusimamia maendeleo ya wananchi nyie mnagombana." amesema Waziri Mkuu

Aidha Waziri Mkuu amesema, "sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara, mkandarasi na mhandisi mshauri wote wanaonekana hawapo makini katika kufanya kazi hii."

Post a Comment

0 Comments