WhatsApp: Kuja na njia ya kuzuia kuingizwa kwenye makundi ya WhatsApp hovyo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 24, 2019

WhatsApp: Kuja na njia ya kuzuia kuingizwa kwenye makundi ya WhatsApp hovyo
whatsapp WhatsApp: Kuja na njia ya kuzuia kuingizwa kwenye makundi ya WhatsApp hovyo
Imeripotiwa na vyanzo mbalimbali ya kwamba WhatsApp wapo kwenye hatua za mwisho wa kuwezesha watumiaji wake kuwa na uwezo wa kuzuia kuingizwa kwenye makundi (Groups) hovyo hovyo.
Katika kuwezesha hilo katika eneo la ‘Settings’ kwenye WhatsApp wataongeza sehemu mpya itakayopatikana kwa kupitia Settings>>Account>>Privacy>>Groups
Kuja na njia ya kuzuia kuingizwa kwenye makundi ya WhatsApp hovyo
Wasiopenda kuingizwa kwenye magroups bila ridhaa yao hii ni habari njema sana
Utakapofika hapo kuna kuwa na uchaguzi wa aina tatu katika eneo la ‘who can add me to groups’ yaani ‘Nani anaweza kukuingiza kwenye kundi’ yaani ‘.
  • Everyone – Mtu yeyote
  • My Contacts – Watu ambao una namba zao za simu
  • Nobody – Yaani kusiwe na mtu mwenye uwezo huo. Ukichagua hapa kutakuwa hakuna mtu anayeweza kukuingiza kwenye kundi lolote labda hadi wewe mwenyewe ujiunge na kundi kwa njia ya kubofya linki za groups. Na linki hii itakuwa inayotoka kwa Admin wa kundi na itakuwa inafutika (expire) ndani ya masaa 72.
whatsapp groups
Muonekano wa machaguo

Inasemekana uwezo huu mpya utakuja muda wowote kuanzia sasa kwa watumiaji wote wa WhatsApp.

Je unadhani huu ni uwezo muhimu kwako? Tuambie kwenye comment.

Vyanzo: NewsMinute, Google News na vyanzo mbalimbali
Loading...

No comments: