Yanga yapata pigo kwa kufiwa na kiongozi wake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 24, 2019

Yanga yapata pigo kwa kufiwa na kiongozi wake


Yanga yapata pigo kwa kufiwa na kiongozi wake
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Mustapha Urungu, amefariki dunia mchana wa leo Jumamosi Februari 23, 2019 nyumbani kwake Temeke.

Msemaji wa Yanga Dismas Ten amethibitisha taarifa hizo kwa kusema Urungu amefariki dunia akiwa nyumbani kwake na chanzo ni presha kushuka.

Ten ameongeza kuwa kwa mujibu wa familia ya marehemu Urungu ni kwamba aliamka akiwa sawa lakini ghafla mchana leo alizidiwa na kufariki dunia.

Mwili wa Urungu utasafirishwa kwenda kwao Wilayani Rufiji mkoani Pwani kwaajili ya mazishi ambayo yatafanyika kesho Jumapili.

Ndani ya Yanga Urungu alikuwa na nafasi mbili ambazo ni makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano pamoja na makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili.
Loading...

No comments: