YANGA YAWATULIZA MASHABIKI WAKE, WATOA AHADI NZITO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, February 9, 2019

YANGA YAWATULIZA MASHABIKI WAKE, WATOA AHADI NZITO


NAHODHA wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu amewataka mashabiki wa Yanga wasiwe na presha baada ya kikosi hicho kupoteza pointi saba katika mihezo yake mitatu ya Ligi Kuu Bara.

Yanga walipoteza pointi tatu katika mchezo wao wa kwanza mbele ya Stand United kwa kufungwa bao 1-0, wakalazimisha sare mbele ya Coastal Union ya kufungana bao 1-1 na kutoka suluhu na Singida United Namfua hali iliyopelekea kupoteza pointi saba.

Ajibu amesema wanatambua mashabiki wanahitaji matokeo mazuri hicho ndicho ambacho wachezaji wanafikiria hivyo watafanya maajabu katika michezo yao inayofuata ikiwa ni pamoja na ule dhidi ya JKT Tanzania.

"Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri, kupoteza pointi ni kitu ambacho kinatuumiza ila tutapambana ilitufanye vizuri, mashabiki watupe sapoti," amesema Ajibu.

Yanga ni kinara wa ligi akiwa na pointi 55 baada ya kucheza michezo 22, kesho atakuwa uwanja wa Mkwakwani akikabiliana na JKT Tanzania.
Loading...

No comments: