AGUERO MCHEZAJI BORA WA MWEZI, PEP KOCHA BORA WA MWEZI EPL, GOLI LA SCHAR Vs BURNLEY LAWA GOLI BORA LA MWEZI. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 9, 2019

AGUERO MCHEZAJI BORA WA MWEZI, PEP KOCHA BORA WA MWEZI EPL, GOLI LA SCHAR Vs BURNLEY LAWA GOLI BORA LA MWEZI.


Hakika mwezi Februari ulikuwa mwezi mzuri sana kwa Manchester City ambao walikuwa wakipunguza gap la point dhidi ya Liverpool na hatimaye kurudi kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Premier League. 

Straika wa timu hiyo Muargentina, Sergio 'Kun' Aguero ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Fabruari kwa Ligi hiyo huku kocha wake Pep Guardiola akitwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi Februari wa Ligi kuu ya Uingereza baada ya kushinda mechi nne kati ya nne ikiwemo mechi ya ushindi wa 6-0 dhidi ya Chelsea. Aguero ameshinda tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika michezo minne aliyocheza mwezi huo, huku akifunga magoli 7 na kuisaidia timu yake kushinda michezo hiyo yote. 

Pamoja na hayo, goli la Beki wa Newcastle United Fabian Schar dhidi ya Burnley limechaguliwa kuwa Goli bora la Mwezi Februari katika Ligi Kuu ya Uingereza. 
Loading...

No comments: