ALEXIS SANCHEZ NJE WIKI 6 HADI 8, AONGEZA ORODHA YA MAJERUHI WA UNITED - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 4, 2019

ALEXIS SANCHEZ NJE WIKI 6 HADI 8, AONGEZA ORODHA YA MAJERUHI WA UNITED


Alexis Sachez atakuwa nje ya dimba kwa muda wa mpaka miezi miwili baada ya kuumia goti kwenye mechi ya ushindi wa United wa 3-2 dhidi ya Southampton siku ya Jumamosi. 

Kwa muda huo wa nje ina maana kwamba Sanchez atakuwa nje mpaka mwishoni mwa mwezi wa nne na kuibua mashaka kama atacheza tena msimu huu. 

Alexis ameongeza idadi ya wachezaji wa United majeruhi ambao ni Anthony Martial, Jesse Lingard, Ander Herrera na Nemanja Matic. Paul Pogba pia atakosekana kutokana na adhabu kwenye mechi ya UEFA dhidi ya PSG. 

Jeraha la Sanchez limekuja kwenye wakati mbaya zaidi ndani ya United. 
Loading...

No comments: