ALIYEKUWA MENEJA WA KAMPENI ZA DONALD TRUMP 2016 AFUNGWA JELA


Taarifa zilizotufikia ni kuwa bwana Paul Manafort (69) ambaye alikuwa ni meneja wa kampeni za Uraisi za Donald Trump mwa ka 2016, amefungwa miezi 47 jela sawa na miaka 3 na miezi 11 baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi na udanganyifu wa kibenki. 

Hii sio mara ya kwanza kwa Manafort kukutwa na hatia kwani mwaka jana alikutwa na hatia ya kuficha mamilioni ya dola alizozipata baada ya kufanya kazi za kisiasa nchini Ukraine. 

Inaelezwa kuwa wiki ijayo huenda akasomewa hukumu nyingine kwa makosa ya kufanya ushawishi haramu wakati wa kampeni. 

Post a Comment

0 Comments