AMBER RUTH AFUNGUKA HAYA KUHUSU KURUDI SHULE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 25, 2019

AMBER RUTH AFUNGUKA HAYA KUHUSU KURUDI SHULE

Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Ruth’ amesema ameamua kurudi shule baada ya kugundua elimu ni kila kitu anachokihitaji kwa sasa katika maisha yake.

Amber Ruth

Akizungumza na East Africa TV, Amber Ruth, amesema kwamba kutokana na matatizo mengi aliyopitia ameamua kurudi shule kwani ndiko sehemu ambayo anaona anapata amani ya moyo ikiwa ni pamoja na kupoteza Stress.

 Mwanadada huyo asiyekaukiwa matukio amesema kwamba baada ya kuacha shule 2009 akiwa kidato cha pili, kwa sasa ameanza kidato cha tatu katika shule ya kulipia yeye na mume wake.

 Sababu nyingine iliyomfanya Amber Ruth kurudi shule ni kutaka kufahamu vizuri lugha ya kingereza kwa kuwa inamsumbua sana hasa anapokutana na watu wasiojua lugha ya kiswahili.

Akizungumzia kuhusu wanafunzi wengine wanavyomchukulia, Amber anasema japo wapo watu wengine wanaombeza kwa kitendo kilichowahi kumtokea lakini ni tofauti na kushinda mtaani ambapo ndipo kunampelekea hadi kulewa ili kupoteza mawazo.


Kuhusu kuacha kushiriki matamasha ya usiku, amesema atazidi kushiriki kwa kuwa ndipo anakopatia fedha za matumizi mbalimbali na shule anayosoma haimzuii kufanya hayo.

Chanzo:Eatv.tv
Loading...

No comments: