Athari za Mkazo (Stress) kwa Mwili & Afya Yako! - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 2, 2019

Athari za Mkazo (Stress) kwa Mwili & Afya Yako!

Watu wenye mkazo (stressed-out people) mara kwa mara wanakuwa na ubongo mdogo. Viwango vikubwa vya homoni cortisol (homoni ya mkazo) hupunguza ujazo wa ubongo na uwezo wa ubongo kufanya kazi.

 Athari Zingine za Mkazo (Stress):-

1: Huharibu usingizi!
Mkazo hufanya akili kukumbwa na wasiwasi mwingi. Mawazo mengi hufanya mtu akose usingizi. Na kukosa usingizi humfanya mtu awe na mkazo zaidi.


2: Hufanya ngozi kuonekana mbaya!
Watafiti wanadai mkazo huamsha matatizo kama chunusi, upara na kizema (mzio unaofanya ngozi kuvimba). Na ikiwa mtu ana matatizo haya toka mwanzo yanaweza kushamiri zaidi. Mkazo pia hufanya vidonda kuchelewa kupona.3: Ni hatari kwa afya ya moyo!
Kila kipindi ambacho mtu anakuwa na mkazo, homoni ya adrenalini hutokezwa ambayo huongeza mapigo ya moyo na shinikizo la damu.4: Huharibu mfumo wa umeng'enyaji wa chakula!
Ubongo na mfumo wa umeng'enyaji wa chakula wa mtu unaendeshwa na homoni zinazofanana sana. Hivyo, ubongo ulio na mkazo wakati mwingine husababisha kiungulia, vyakula kutomeng'enywa vizuri, kuhara, kichefuchefu na kutapika.5: Huongeza hatari ya mtu kuugua!
Tafiti moja ilidai watu walio na mkazo sugu wana hatari mara mbili ya kuugua mafua na kikohozi.Nini Unaweza Fanya Kuepuka Mkazo?
Madaktari wanasema ulaji chakula bora kiafya hasa matunda na mboga za majani husaidia sana. Pia, wanashauri kuushughulisha mwili kwa mazoezi na kusinzia angalau masaa 8 kila usiku.

Loading...

No comments: