Azania Bank yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuungana na wanawake katika Taasisi ya Saratani Ocean Road - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 10, 2019

Azania Bank yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuungana na wanawake katika Taasisi ya Saratani Ocean Road


Wafanyakazi wanawake wa Azania Bank watoa zawadi na misaada mbalimbali kwa wanawake wenzao wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kama sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.


Meneja Mwandamizi wa Uendeshaji wa Azania Bank, Jane Chinamo akizungumza na wanahabari  baada ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo kutoa zawadi na misaada mbalimbali kwa wanawake wenzao  wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kama sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

Dar es Salaam, 9 Machi 2019:Wafanyakazi wanawake wa Azania Bank leo wameungana na wanawake wenzao wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kama sehemu ya kuonyesha upendo na mshikamano katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019. Ziara ya Wanawake wa Azania Bank katika wodi za wanawake wanaopatiwa matibabu katikaa taasisi hii imelenga kuwapa moyo wagonjwa na kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya kujikimu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja Mwandamizi wa Uendeshaji wa Azania Bank, Jane Chinamo amesema, “Tuko hapa leo ili kusherekea siku hii maalum pamoja na wanawake wenzetu ambao tunawahitaji sana waweze kurejea katika afya zao ili waendeleze maisha yao pamoja na ya wapendwa wao. Kama benki, ni jukumu letu la msingi kuchangia katika kuboresha uchumi wa taifa, na hilo linaweza kufanikiwa tu pale tutakapokuwa na jamii zenye watu wenye afya bora ili waweze kusaidiana katika kulifikia lengo la kuwa na maisha yenye mafanikio”.
Katika kuwatakia kupona haraka, Chinamo amesema wanawake wana mchango mkubwa katika jamii na kwamba wamekuwa mstali wa mbele katika juhudi za kuliletea taifa maendeleo. Kauli mbiu katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa mwaka huu ni ‘Usawa kwa Maendeleo’ #BalanceForBetter
Katika ziara hiyo, wanawake wa Azania Bank wametoa zawadi na misaada mbalimbali kwa wagonjwa pamoja na vifaa tiba kwa wauguzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka ili kutambua na kupongeza mchango wa wanawake katika nyanja za kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Siku hiyo pia hutumika kama mojawapo ya njia za kuikumbusha dunia juu ya umuhimu wa usawa wa kijinsia.
MWISHO//
Loading...

No comments: