BAADA YA KUTOLEWA UEFA, EUSEBIO DE FRANCESCO AFUNGIWA VIRAGO NA AS ROMA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 8, 2019

BAADA YA KUTOLEWA UEFA, EUSEBIO DE FRANCESCO AFUNGIWA VIRAGO NA AS ROMA


Klabu ya AS Roma imemfuta kazi aliyekuwa kocha wao Eusebio De Francesco baada kupoteza mchezo wa marudiano dhidi ya FC Porto na kutupwa nje ya michuano ya UEFA Champions League katika hatua ya 16 bora. 

Awali wiki iliyopita fununu zilianza kuzagaa kuhusiana na mpango wa klabu hiyo kumfukuza kazi kocha huyo lakini ilitegemea na matokeo ambayo angeyapata katika mechi hiyo ya marudiano ya hatua ya mtoano dhidi ya Fc Porto. 

De Francesco atakumbukwa kwa mengi ikiwemo kuichapa FC BARCELONA 3-0 msimu uliopita katika mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa Ulaya huku wakiwa wamechapwa 4-1 kabla ya mechi hiyo na kuiwezesha Roma kutinga Nusu fainali. 

Loading...

No comments: