Babu TALE Afunguka "Ruge Ukweli Utabaki Kuwa Ukweli Tulipishana Eneo la Biashara Sababu ya Kibinadamu" - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 1, 2019

Babu TALE Afunguka "Ruge Ukweli Utabaki Kuwa Ukweli Tulipishana Eneo la Biashara Sababu ya Kibinadamu"


From @babutale -  Pumzika kwa Amani Kaka, ndio neno pekee naloweza kusema juu yako mengine haya yanaongezeka ni ya Dunia, ikiwa ni sifa na ulichonifanyia kwenye maisha yangu? nilishapost ukiwa hai na nakumbuka tulikua pamoja na ukaniambia Asante maana ni wachache wenye kusifia watu wakiwa hai. Nenda kaka nitaendelea kuenzi na kulinda ahadi niliyokupa. Nakumbuka uliniambia katika maisha yangu kitu pekee nikifanya kitakachokufanya utanichukia mpaka siku yako ya kufa ni kumuuzi mke wangu maana amenizalia watoto wawili tena wote wakiume na ulikua ukiniita Baba THT kwa maana ya majina ya wanangu Tale Hamisi Taletale (THT). Kwenye hili jambo nitakuwa tofauti na wapenda kiki kuonekana wameguswa na msiba wakati inawezekana tangu wasikie umetangulia hawajakaa hata sekunde moja kukuombea kwa Mungu akuweke mahala pema meponi.

Ruge ulikuwa binadamu na sio malaika, sasa ukiwa binadamu na ukose kumkosea mtu hiyo ni ndoto tena ya alinacha, ukweli utabaki kua ukweli tulipishana kwenye eneo la biashara hii yote sababu za kibinadamu, hazinipi nafasi hata chembe ya kunizuia kukuombea kwa Mungu akuweke mahala pema peponi kwa mengi mema uliyoyafanya. Waliopost na wasipost aimsanishi kua hiyo ndio dua kwa marehemu, sote tunajua dua utoka moyoni sio mtandaoni.  Pumzika Kwa Amani Kaka!
Loading...

No comments: