BALE AITAJA ARSENAL - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 23, 2019

BALE AITAJA ARSENAL


GARETH Bale ametoa kauli ambayo inaweza isiwe nzuri kwa mashabiki wa timu yake ya zamani ya Tottenham, ambapo amedai kuwa alikuwa akiitazama sana Arsenal wakati anakua.

Nyota huyo wa Real Madrid ameyasema hayo wiki hii alipokuwa katika kipindi maalum cha kuonyesha jezi, kauli hiyo siyo nzuri kwa Tottenham kwa kuwa Arsenal ni wapinzani wao wa jadi na mchezaji huyo amekuwa akihusishwa kuondoka klabuni kwake mwishoni mwa msimu huu.

Bale amesema yeye alikuwa ni shabiki mkubwa wa Thierry Henry na Dennis Bergkamp na kueleza kuwa walikuwa wakimvutia walipokuwa wakiichezea Arsenal. Mbali na kutoa kauli hiyo, pia aliitoa akiwa ameshika jezi ya Arsenal yenye jina la Henry.

“Nilikuwa naitazama sana Arsenal na nilikuwa naburudika kumtazama Henry na Dennis Bergkamp, nasema hivyo lakini najua mashabiki wa Tottenham hawatakuwa na furaha kwa mimi kuishika hii jezi.

Aidha, kuhusu uhusiano wake na Cristiano Ronaldo wa Juventus ambaye walikuwa naye Real Madrid alisema hajawahi kuwa na tatizo naye, kuhusu chuki iliyodaiwa kuwepo alisema vyombo vya habari ndivyo vimekuwa vikikuza mambo.

“Cristiano ni mchezaji mzuri, nimefurahi kucheza naye pamoja, vyombo vya habari vinakuza mambo ambayo hayapo, alifanya mambo mengi mazuri klabuni, mabao aliyofunga na anaendelea kufanya vizuri.”
Loading...

No comments: