BENKI YA AZANIA YAWAHAKIKISHIA WATEJA WAKE UBORA WA HUDUMA BAADA YA KUINUNUA 'BANK M' - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 20, 2019

BENKI YA AZANIA YAWAHAKIKISHIA WATEJA WAKE UBORA WA HUDUMA BAADA YA KUINUNUA 'BANK M'

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya hatua ya benki yake kuinunua Bank M.

Benki ya Azania leo imewahakikishia wateja wake kuwa itaendelea kutoa huduma za ubora wa hali ya juu kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa kipindi kirefu sasa. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari. Hii ni baada ya Benki kuu ya Tanzania (BoT) kutoa tamko kuhusiana na kukamilika rasmi kwa mchakato wa kuhamishia Mali na Madeni ya iliyokuwa Benki M na kuzihamishia benki ya Azania 

Tumeingia kwenye makubaliano na BoT ya kuinunua benki M ya Dar es Salaam hatua ambayo itapanua soko letu katika sekta ya kifedha hapa nchini Tanzania. Ununuzi huu wa benki M unatarajiwa kuongeza ufanisi kupitia michakato iliyoboreshwa, utamaduni na kuongeza soko. Itembe amesema. 

Mnamo Agosti 2018, BoT iliiweka benki M chini ya uangalizi maalum kutokana na beki hiyo kushindwa kutoa huduma za kifedha kwa mujibu wa sheria inayosimamia mabenki. 

Ununuzi huu umefanikiwa baada ya benki ya Azania kutuma maombi na andiko kwenda BoT juu ya nia yake ya kuinunua Benki M, baada ya hapo majadiliano marefu baina ya wanahisa na Benki Kuu yaliendelea kwa miezi kadhaa. Benki ya Azania kupitia kwa wanahisa wake wakubwa ambao ni PSSSF (51.95%), NSSF(27.99%), EADB(0.51%),Wanahisa wadogo (0.34%) pamoja na wanahisa wapya (National Health Insurance Fund(17.42%) na Workers Compensation Fund (1.79%)) hatimae kufikia muafaka wa upatikanaji wa mtaji na ukwasi wa uendeshaji wa benki baada ya kuichukua Benki M. 

Itembe amesema aina hii ya ununuzi wa benki inajulikana kama “sheria ya uchukuzi wa kiutendaji” 

"Tuliona ununuzi wa benki hii ni muhimu kwa utendaji za benki ya ABL. Ukamilisho wa uambatanisho wa benki hizi mbili unatarajiwa kukamilika siku 45 kwanzia siku tulio ingia katika makubaliano ya mkataba wa ununuzi na BOT (Ijumaa, 15.03.2019). Tutatangaza rasmi siku ya ufunguzi wa tawi amabalo wateja wetu w Benki M wataendelea kupokea huduma bora kufikia 

matarajio yao kupitia mtandao na matawi ya Benki ya Azania na matawi matatu amabayo awali yalikuwa wakimilikiwa na Benki M.’’ Amesema 

Uamuzi wa kupewa taasisi hiyo ulifanywa katika mkutano wa mwaka ulifanyika Desemba 21, 2018 ambapo wanahisa walikubaliana kuongezea mtaji Benki ya Azania na kukaribisha wanahisa wapya ambao nao pia walikubali kuongeza mtaji iliyofanya Azania kuwa imara na kuweza kuipata Benki M. Uchukuzi huu umeipeleka Azania mbali zaidi kuongeza idadi ya matawi kutoka 19 hadi 22 na kuongeza mtaji wake kutoka billion 64 za kitanzania mpaka billion 181 za kitanzania wakati jeduwali la mizani kuvuka trilioni kutoka awali ambapo ilikuwa nusu trilioni. 

“Baada ya kipindi hiki cha siku 45 tunatarajia kufungua milango kwa wateja wote wa Benki M ambao watahudumiwa katika tawi lolote la ABL watakalopendelea nchini Tanzania. Pia mchakato huu utapelekea kubadili mwonekano wa matawi ya benki M ya Kisutu, Pugu na Arusha ili yafanane na yale ya benki ya Azania” amesema Itembe. 

Wanahabari wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe wakati akiwataarifu juu ya hatua ya Bank M kununuliwa na Benki ya Azania.

Kwa mujibu wa Itembe, hatua hii mpya inaifanya ABL kuwa (Tier One bank) kwa namna yoyote ile haitabadilisha muundo wa utendaji kazi wa benki badala yake utaunganisha mifumo hii miwili. 

“Kama sehemu ya uendeshaji, Benki ya Azania itaendelea na utekelezaji wa mikakati yake ya kisera ya miaka mitano (Five-Year strategic plan) ambayo itafanyiwa maboresho ili kuendana na huu Muunganiko wa Benki hizi mbili. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha wateja wa iliyokuwa Bank M wanaendelea kupata huduma zilizo bora zaidi”. 

Mkurugenzi wa ABL pia amebainisha kuwa ni mpango wa benki kuendelea kufanya kazi kwa kutengeneza timu moja ambapo wafanyakazi wa Azania na wale waliokuwa wa benki M watachanganywa katika maeneo mbalimbali ya kazi na kukuza utamaduni wa utendaji bora na utawala bora. 

Itembe pia amesema kazi itaanza mara moja kutokana na alichokiita muunganiko mzuri wa Benki zote mbili kuwa na mfumo wa tehama unaoendana kwa kiasi kikubwa. hivyo haitakuwa ngumu sana kuhamisha taarifa (data) 

Pia Benki ya Azania imesema itaendelea kufanya maboresho na kutumia teknolojia ya kisasa ili katika kuwahudumia wateja wakubwa na wadogo kwa ubora na ufanisi zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe akijibu maswali ya wanahabari wakati akiwataarifu juu ya hatua ya Bank M kununuliwa na Benki ya Azania mapema leo jijini Dar es Salaam.


Loading...

No comments: