BODI YA NYAMA KUANZISHA OPERESHENI YA KUKAMATA NA KUCHOMA MAGOGO YA KUKATIA NYAMA MABUCHANI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 7, 2019

BODI YA NYAMA KUANZISHA OPERESHENI YA KUKAMATA NA KUCHOMA MAGOGO YA KUKATIA NYAMA MABUCHANI


Bodi ya nyama Tanzania, inatarajia kuanzisha Operesheni nchi nzima ya kukamata na kuchoma magogo yanayotumika kukatia nyama kwenye mabucha ikisema kuwa kufanya hivyo kutasaidia watumiaji wa kitoweo hicho, kula nyama ambayo haina uchafu wowote.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama, Imani Sichalwe kwenye Mkutano Mkuu wa shirikisho la wanachama wa biashara ya mifugo na nyama Tanzania (TALIMETA), uliofanyaka Jijini Dodoma ambapo akijibu hoja ya Mwenyekiti wa wauza nyama Jijini Arusha Alex Lasiki kuhusu upatikanaji wa mashine za kukatia nyama nchini.

Akijibu hoja hiyo, Sichalwe amesema wafanyabiashara hao wanatakiwa kuyaondoa magogo hayo mara moja na kutumia mashine za kukatia nyama na kwamba mashine hizo zinapatikana nchini kwa gharama nafuu.

Akizungumzia juu ya wafanyabiashara wanaouza nyama kwenye ndoo Sichalwe amesema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, huku akitumia nafasi hiyo kuwataka wenye tabia hiyo kuacha mara moja.

Kwa upande wake Afisa nyama wa Bodi hiyo Edgar Mambo, amesema nyama ikikatwa kwenye Gogo na kuhifadhiwa kwenye Friji baada ya muda hubadilika rangi kutokana na uchafu unaokuwepo kwenye gogo hilo.

Katibu mkuu wa TALIMETA, Raphael Chacha amebainisha baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na usimamizi hafifu wa machinjio nchini unaoruhusu uuzaji holela wa nyama na kupelekea wao kupata hasara na kufilisika.

Loading...

No comments: