Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo Amchapa Sergio wa Argentina - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 24, 2019

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo Amchapa Sergio wa Argentina


Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amempiga bondia wa Sergio Gonzalez Argentina kwenye mpambano wa dondi uliyofanyika usiku wa jana jumamosi jijini Nairobi Kenya.


Ilichukua hadi raundi ya tano ambapo Mwakinyo alifanifikiwa kumchapa Muargentina huyo kwa technical knockout ‘TKO’ baada ya kumtwanga makonde ya nguvu mpinzani wake mpaka akapoteza muelekeo na kuanguka chini nakushindwa kuendelea na mpambano.

Akiongea muda mfupi baada ya ushindi huo Mwakinyo aliwashukuru watanzania na wadhamini wake nkuitakia kheri Timu ya taifa starts kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Uganda.

“Nafuraha sana kwa ushindi wangu mkubwa leo nashukuru sana Mwenyezi Mungu nashukuru watanzania wote waliokuwa wakiniombea. Na pia ushindi wangu wa leo ukawe mfano kesho kwa Taifa stars katika mechi yao ngumu”. Mwakinyo aliongea.

Hongera sana bondia Hassan Mwakinyo kwa ushindi huo.

Uganda Watuma Salamu kwa Taifa Stars

No comments: