Burundi yafuzu AFCON kwa Mara ya Kwanza na Kuungana na Timu Nyingine 18, - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 24, 2019

Burundi yafuzu AFCON kwa Mara ya Kwanza na Kuungana na Timu Nyingine 18,


Burundi yafuzu AFCON kwa Mara ya Kwanza na Kuungana na Timu Nyingine 18,
Jana Machi 23, 2019 Burundi imefanikiwa kufuzu michuano ya AFCON 2019 kwa mara ya kwanza katika historia kwa kupata sare ya 1-1 dhidi ya Gabon.


Kwa matokeo hayo Gabon inayoongozwa na Aubameyang imetupwa nje ya michuano hiyo, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Juni mwaka huu nchini Misri.

Mpaka sasa ni mataifa 19 yamefuzu michuano hiyo, huku mataifa mengine matano yakisubiriwa kufuzu leo ili kukamilisha timu 24 zitakazoenda Misri kwenye michuano hiyo.


Leo Tanzania inatupa karata yake ya mwisho kwenye nafasi ya kuwania kufuzu dhidi ya Uganda, ambapo itahitaji matokeo ya ushindi kwanza na baadae waombee Cape Verde waifunge Lesotho au mchezo huo kati ya Lesotho na Cape Verde utoke droo.

Kwa hiyo Taifa Stars hata ikishinda dhidi ya Uganda, halafu Lesotho nayo ikashinda basi tutakuwa tumetolewa kwani Lesotho atakuwa na pointi 8 na Tanzania pointi 8 ila rekodi ya Head to Head, Taifa Stars imepigwa zaidi na Lesotho.

Taifa Stars iliruhusu sae hapa Tanzania na kukubali kichapo nchini Lesotho, hivyo leo Watanzania wanatakiwa waiombee Cape Verde ishinde dhidi ya Lesotho na Taifa Stars ishinde dhidi ya Uganda. 

No comments: