#CHUKUA HII;Wanawake hutegemea zaidi furaha kutoka kwa waume zaoDaktari wa falsafa na mshauri wa masuala ya ndoa nchini Dkt. Ellie  V.D Waminian, ameeleza kuwa  wanawake  hutegemea zaidi furaha kutoka kwa waume zao na wakikosa huduma hiyo,matokeo yake ni kukosa kujiamini.

Dkt Ellie amesema kuwa mwanamke siku zote hana imani kama anapendwa na tegemeo kuu la mwanamke  ni furaha, na si upendo kama watu wengi wanavyofikiri.

“Mwanamke ana mapenzi ila hana upendo, mwanamke hapendi bure bali anapenda kwa mazao, na zao kuu analolitegemea ni furaha na kicheko. Mwanamke anapenda maneno mengi mazuri ndiyo maana anaongea zaidi ya maneno 'maximum' 25,000  kwa siku, na mwanaume 'maximum' yake ni maneno 12,500”. Amesema Dkt. Ellie

Aidha, Dkt Ellie ameongeza kuwa katika mapenzi au upendo  suala la mazoea ni moja ya chanzo cha migogoro katika mahusiano na njia kuu ya kuepuka migogoro ni kuwepo umbali kati ya wapenzi hata kwa muda mfupi wa masaa kadhaa kwa siku na pia kuwepo kujali na kuthaminiana.

Pia kulingana na utafiti wa Daktari na Mshauri  wa Masuala ya Ndoa na Mwakilishi kutoka  taasisi ya Best Life ya New York  nchini Marekani Melissa Divaris Thomposon, imeelezwa kuwa mwanamke hupenda kusikia maneno yafuatayo; 'Unajua kwamba nakupenda, uko sahihi, usiku wa jana ulikuwa mzuri, nakupenda ukiwa hujapaka make- up, ukweli ni kwamba huonekani kuwa mnene, nakupenda jinsi ulivyo, sielewi ila nitajaribu. Maneno kama hayo ndio humfanya mwanamke kuwa na furaha zaidi na kufurahia mahusiano

Post a Comment

0 Comments