CONOR McGREGOR AKAMATWA KWA KOSA LA KUHARIBU SIMU YA SHABIKI, ATOLEWA KWA DHAMANA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 12, 2019

CONOR McGREGOR AKAMATWA KWA KOSA LA KUHARIBU SIMU YA SHABIKI, ATOLEWA KWA DHAMANA


Miezi mitano baada ya mpiganaji Conor McGregor kumaliza adhabu yake ya huduma za jamii kwa kosa la kushambulia basi, mbabe huyo wa UFC ameingia kwenye matatizo na sheria.

Kwa mujibu wa mtandao wa Miami Herald, Conor amekamatwa usiku wa kuamkia leo mjini humo baada ya kuvunja simu ya shabiki mmoja ambaye alikuwa akitaka kupiga picha, aliipora simu hiyo na kuiharibu. Imetajwa kuwa na thamani ya Tsh. milioni 2 za Kitanzania.

Sasa baada ya tukio hilo, polisi walitazama kamera za eneo hilo na kumbaini Mcgregor, walimfata kwake na kumkamata. Ameshtakiwa kwa kosa la jinai kwa ukabaji na kosa dogo la uhalifu.

Baadaye kidogo zilitoka taarifa kuwa Conor ameachiwa kwa dhamana. 
Loading...

No comments: