CRISTIANO RONALDO MATATANI KWA AINA YA USHANGILIAJI WAKE DHIDI YA ATLETICO MADRID - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 19, 2019

CRISTIANO RONALDO MATATANI KWA AINA YA USHANGILIAJI WAKE DHIDI YA ATLETICO MADRID


Cristiano Ronaldo amefunguliwa mashitaka na Shirikisho la soka barani ulaya UEFA,  kutokana na ushangaliaji wake kwenye mechi ya hatua ya 16 ya juventus dhidi ya Atletico Madrid. 

Ronaldo alishangalia kwa kuiga ushangiliaji wa kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone kwa kushika korodani zake. Ikumbukwe kuwa baada ya kufanya hivyo kwenye mechi ya kwanza kule Hispania, kocha Diego Simeone alipigwa faini ya Pauni 17,000 pamoja na kuomba radhi kwake alikokufanya ili aepuke faini. 

Kamati ya Maadili na Nidhamu ya UEFA itafanyia kazi kesi hii March 21. Juventus watacheza mechi ya kwanza ya hatua ya robo fainali dhidi ya Ajax jijini Amsterdam Aprili 10. 
Loading...

No comments: