Dereva wa Mwendokasi kizimbani kwa kumkata Abiria kidole - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 1, 2019

Dereva wa Mwendokasi kizimbani kwa kumkata Abiria kidole


DEREVA wa basi la Mwendokasi, Khalid Shaha (43), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam, akikabiliwa na shtaka la kumkata kidole Godfrey Liwa kwa kioo cha gari.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Hanifa Mwingira, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Matarasa Hamisi, alidai Oktoba 12 mwaka jana eneo la Magomeni, Wilaya ya Kinondoni, dereva huyo alimkata Liwa kwa kioo cha gari.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na aliachiwa kwa dhamana hadi Machi 12, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

Wakati huo huo, watu wawili; Ester Stephen (56) na Andrew Mkuta (51), wakazi wa Tandale Mkunduge, Wilaya ya Kinondoni, wamepandishwa kizimbani kwa shtaka la kukutwa na lita tano za gongo.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Bonifasi Lihamwike, Wakili wa Serikali, Veronika Mtafia alidai Novemba 14 mwaka jana eneo la Tandale kwa Mkunduge, Wilaya ya Kinondoni, walikutwa na gongo.

Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo na walirudishwa rumande hadi Machi 3, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.
Loading...

No comments: