Donald Trump Atishia Kufunga Mpaka wa Marekani na Mexico - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 31, 2019

Donald Trump Atishia Kufunga Mpaka wa Marekani na MexicoRais wa Marekani, Donald Trump ametishia kufunga mpaka wa Marekani na Mexico ikiwa Mexico hawatachukua hatua madhubuti kuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.

Hatua hiyo ya kufunga mpaka inatishia kupoteza biashara yenye thamani ya mabilioni ya dola za kimarekani.

Tishio hilo limekuja baada ya kuwepo kwa wimbi kubwa la wahamiaji wanaoingia Marekani wakitokea Mexico kwa nia ya kutafuta hifadhi.

Waziri wa mambo ya nje Marcelo Ebrard amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Mexico ni ''jirani mzuri'' kwa Marekani ''lakini haitachukua hatua kutokana na vitisho''.
Loading...

No comments: