DOOH! SERIKALI YA DUBAI YAMKANA R. KELLY - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 26, 2019

DOOH! SERIKALI YA DUBAI YAMKANA R. KELLY


WIKI iliyopita mwanamuziki wa Marekani, R. Kelly, aliiomba mahakama mjini Chicago impatie ruhusa ya kwenda mjini Dubai kufanya maonyesho yake kadhaa ambayo alidai  kutumbuiza kabla ya kutiwa nguvuni.

Hata hivyo, serikali ya Dubai imekanusha kuwa mwanamuziki huyo hana onesho lolote mjini humo. Imesema:  “Mamlaka mjini Dubai haijapokea ombi lolote la onyesho kutoka kwa R. Kelly na hakuna ukumbi wowote ambao umewekewa oda (booked).”

Mwanasheria wa Kelly. Steven A. Greenberg. amejibu taarifa hiyo kwa barua pepe kwenda  The Associated Press kwamba: “Kelly alikuwa na mkataba na mchakato wote umo kwenye mkataba huo. Hatukusema kuwa alialikwa na familia ya kifalme…”

R. Kelly alikumbwa na makosa kumi ya unyanyasaji wa kijinsia mwezi uliopita, kabla ya kutolewa jela mwezi huu kwa dhamana ya Dola 100,000 (Tsh. mil. 234.5).


Loading...

No comments: