Fahamu Kama Upo Kwenye Hatari ya Kupatwa na Kiharusi (Stroke)! - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 3, 2019

Fahamu Kama Upo Kwenye Hatari ya Kupatwa na Kiharusi (Stroke)!


Kiharusi (Stroke) ni ugonjwa unaosababisha viungo vya mwili kupooza kutokana & kuvuja damu au kuziba kwa mshipa wa damu katika ubongo. Kiharusi kinaweza kumkumba mtu yeyote lakini watu wazima wenye umri kuanzia miaka 40 na kuendelea ndiyo hushambuliwa zaidi.


Ubongo ukikosa damu kwa masaa 24 ama zaidi chembe hai za ubongo hufa, baada ya kukosa hewa safi na virutubisho vingine. Aina za Kiharusi: Kiharusi cha ubongo kukosa hewa, Kiharusi cha mshipa kupasuka & Kiharusi cha kuziba mshipa wa damu.

Kiharusi cha kukosa hewa kwenye ubongo hutokea pale mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye ubongo kuziba au kusinyaa sana. Mishipa ya damu katika ubongo inaweza kuzeeka, kutanuka na kupasuka, damu kuvilia kwenye ubongo na kusababisha Kiharusi. Mtu mwenye matatizo ya moyo, damu inaweza kuganda kwenye moyo na baadae ikasafirishwa kwenda kwenye ubongo na kiziba huko.


Dalili za Kiharusi: Ganzi au udhaifu unaoanza ghafla. Mara nyingi hutokea upande mmoja wa mwili, yaani kushoto au kulia. Upande mmoja wa uso kufa ganzi au kuwa dhaifu. Kuchanganyikiwa na kushindwa kuongea ghafla tu.Kizunguzungu na wakati mwingine kupoteza fahamu.

Dalili zingine ni kuona kitu kimoja mara mbili au kupoteza nguvu ya kuona inayoweza kutokea jicho moja au yote mawili. Kichwa kinauma sana ghafla na mara nyingine huambatana na kichefuchefu & wakati mwingine kutapika. 

Namna za kuzuia Kiharusi: Pima shinikizo la damu, kama limepanda basi tumia dawa na uishi kiafya ili kudhibiti kupanda. Pima kiwango cha lehemu (kolesteroli) katika mwili wako na kikiwa juu pata matibabu haraka sana. Acha uvutaji sigara kwa maana kemikali kwenye sigara zinaweza kuharibu kuta za mishipa ya damu.
Loading...

No comments: