Fahamu kuhusu Mkutano wa Vijana wa ECOSOC 2019 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 16, 2019

Fahamu kuhusu Mkutano wa Vijana wa ECOSOC 2019

Mkutano wa Vijana wa ECOSOC ni NINI?Kuelekea kwenye jukwa kuu la kisiasa (High-Level Political Forum 2019 au HLPF) litakalofanyika mjini New York mwaka 2019 ambapo nchi mbalimbali zitatuma wawakilishi kutoka serikalini na sekta binafsi tungependa kukuletea makala ya mkutano wa awali ujulikanao kama ECOSOC (The Economic and Social Council), Baraza la Uchumi na Jamii  utakaofanyika huko nchini Marekani kuanzia tarehe 8-9 Aprili 2019.
Wakati pia nchi ipo kwenye mchakato wa kufanya uchambuzi jinsi gani serikali imepiga hatua kutekeleza Malengo 17 ya Umoja wa Mataifa yaani SDGs, Tanzania imengia kwenye huu mchakato kwa mara ya kwanza ambapo maoni (National Voluntary Reviews au VNR) yatakayokusanywa yatajadiliwa kwenye Jukwaa Kuu la kisiasa litakalofanyika mwezi wa saba huku nchini Marekani mnamo mwezi wa saba mwaka huu. 

Jukwaa la Vijana la Uchumi na Jamii (ECOSOC), litakalofanyika mnamo 8-9 Aprili 2019 litatoa jukwaa kwa viongozi vijana kutoka sehemu mbali mbali duniani kushiriki katika majadiliano kati yao na Mataifa ya Wajumbe wa Umoja wa Mataifa (UN) na kushiriki mawazo ya kuendeleza Agenda ya mwaka 2030 ya Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, Ajenda ya Vitendo ya Agosti iliyokubaliwa na viongozi vijana huko Addis Ababa, na Mkataba wa Hali ya Hewa wa Paris (Paris Agreement).

Mkutano huu utakuwa nafasi ya pekee kwa vijana kushiriki ndoto zao na kufafanua michango yao ya msingi kwa mikutano ijayo ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Mkutano wa ECOSOC Youth Forum 2019, Jukkwa  kuu la mwaka 2019 juu ya maendeleo endelevu (High Level Politica Forum) na mikutano mingine ya ngazi za juu yanayotokea karibia na ufunguzi wa Mkutano Mkuu, ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Tatizo la Hali ya Hewa, Mkutano wa ngazi za juu kuhusu Fedha na Maendeleo Endelevu.

Washiriki ni kina nani?

Mashirika mbalimbali yatapekeka viongozi wa vijana kutoka duniani kote kwenda Makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York. Itawapa fursa ya kushirikiana na wawakilishi wa serikali, wajumbe wa vijana, watunga sera na wadau wengine husika katika mashirika ya kiraia na sekta binafsi.

Kwa namna gani huu mkutano unafanyika?

Ni mkutano wa siku mbili utakuwa na vikao vya mjadala, majadiliano maingiliano ya kimazingira na kanda, na kutoa fursa ya kubadilishana maoni mazuri na mawazo juu ya ufumbuzi wa ubunifu juu ya masuala ya umuhimu kwa vijana katika utekelezaji wa agenda ya mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu , na pia juu ya malengo ya maendeleo endelevu chini ya uhakiki katika Baraza kuu la  Kiuchumi na Jamii la Kisiasa mwaka 2019.(HLPF2019)

Tanzania itatuma wawakilishi wa vijana ambao watapata fursa ya kuwakilisha vijana wenzao na kujadili changamoto zinazowakabili vijana na kuangalia uwezekana wa utatuzi wa changamoto hizo.

Usikose kusoma makala hizi kwani tutakuletea makala tu punde mkutano utakapofanyika na kukufahamisha vijana wamejadili nini na ni kitu gani wamejifunza.

Loading...

No comments: