Fahamu Tabia Zinazoharibu Mafigo (Figo) Yako! - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 4, 2019

Fahamu Tabia Zinazoharibu Mafigo (Figo) Yako!

Mafigo hufanya kazi muhimu kwenye miili yetu kama kuondoa sumu, kuchuja damu na kufyonza madini. Uharibifu wa figo unaweza usigundulike kwa miaka mingi kwa maana figo huweza kufanya kazi hata kwa 20% ya uwezo wake.

Tabia zinazoweza kuharibu figo zako:-

Kutokunywa maji ya kutosha. Mafigo huhitaji maji ya kutosha ili kufanya kazi zake kwa ufanisi. Kutokunywa maji ya kutosha kunaweza kusababisha sumu kukusanyika kwenye damu.


Kubana mkojo kwa muda mrefu. Kubana mkojo mara kwa mara huongeza mgandamizo wa mkojo kwenye figo na inaweza kusababisha mawe kwenye figo hata kupelekea figo kushindwa kufanya kazi zake vizuri.Ulaji chumvi nyingi kwenye chakula. Mwili unahitaji chumvi ili kufanya kazi vizuri. Hata hivyo, watu wengi hutumia chumvi nyingi kuliko mahitaji ya mwili kitu kinachosababisha figo kuelemewa hivyo kupandisha shinikizo la damu. Inapendekezwa kutumia gramu zisizozidi 5 kwa siku.Matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi kutia ndani soda. Watu wanaokunywa soda angalau 2 kwa siku wana uwezekano mkubwa wa kuwa na protini kwenye mkojo wao. Protini kwenye mkojo ni moja ya dalili kuwa figo zako hazifanyi kazi kama zinavyotakiwa.Kutopata usingizi wa kutosha. Usingizi wa usiku hauna faida kwako tu bali pia kwenye mafigo yako. Tishu za figo zinafanywa kuwa mpya tena wakati wa usiku hivyo kutolala usiku kunaweza kusababisha uharibifu wa mafigo yako.Matumizi yaliyokithiri ya protini ya wanyama kama nyama nyekundu. Matumizi ya protini ya wanyama mara kwa mara kama nyama ya ng'ombe, nguruwe au mbuzi huongeza mzigo katika ufanyaji kazi wa mafigo, hivyo kuchosha mafigo yako haraka.Matumizi ya pombe. Pombe ni sumu iliyoruhusiwa kisheria inayoweka mkazo (stress) kwenye ini na mafigo inapotumiwa kwa kiwango kikubwa. Kunywa bia moja au gilasi ya mvinyo ni vizuri kwa afya ila kutumia zaidi ya hapo ni hatari kwa afya.
Upungufu wa madini na vitamini mwilini. Mlo wenye matunda na mboga za majani ni muhimu kwa utendaji mzuri wa figo na afya kiujumla. Hatari ya mafigo kuwa na mawe na kushindwa kufanya kazi zake vizuri ni kubwa pale unapokuwa na upungufu wa madini na vitamini. Magnesiamu na vitamini B6 ni muhimu sana kwenye kupunguza hatari ya mawe kwenye mafigo.Loading...

No comments: