Flaviana Matata Aonekana Kwenye Tangazo Jipya la Bidhaa za Rihanna - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 24, 2019

Flaviana Matata Aonekana Kwenye Tangazo Jipya la Bidhaa za Rihanna


Flaviana Matata Aonekana Kwenye Tangazo Jipya la Bidhaa za Rihanna
Mwanamitindo kutokea nchini Tanzania Flaviana Matata ameonekana kwenye tangazo la bidhaa mpya za urembo za mwimbaji Rihanna (Fenty Beauty) . Hii ni baada ya tangazo hilo kupostiwa kupitia ukurasa wa instagram wa Rihanna.

Rihanna amekuwa akiwatumia wanamitindo tofautitofauti katika matangazo ya bidhaa zake hizo za urembo hasahasa wanamitindo wenye asili ya Kiafrika hivyo kwenye tangazo hilo ameonekana Rihanna Flaviana, mwanamitindo Slick Woods na wengine wengi ambapo bidhaa hizo zinatajwa kuwa ziko tayari sokoni tokea March 21,2019.

“Nakushukuru wewe pamoja na timu yako kwa kuniruhusu kuwa mmoja wa hii, najivunia  kwa kila kazi ambayo mnafanya lakini cha muhimu zaidi ni kuwawakilisha wanawake wote, napenda kile ambacho bidhaa zenu zinasimamia” >>> Flaviana Matata

Loading...

No comments: