Fursa kwa Vijana kwenye Kilimo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 4, 2019

Fursa kwa Vijana kwenye Kilimo


Ajira kwa Vijana katika Kilimo kama Suluhisho la Msingi ili kukomesha Njaa na Umaskini Afrika. (Zero Hunger, SDGs 2)

Serikali imewekeza rasilimali fedha kutumika kama fedha za maendeleo ya vijana kutatua tatizo la uhaba wa mitaji ya kuanzia biashara. 
 Maeneo fulani yana fursa za kilimo, biashara na sekta ya huduma lakini vijana hawawezi kuitumia kutokana na uhaba wa mitaji. Serikali imeweka sera ambapo serikali zote za mitaa, vijijini na miji, wanapaswa kutenga asilimia 5 (5%) ya mapato yao ya ndani kama mfuko wa mikopo kwa vikundi yani 'Vikundi vya Kiuchumi vya Vijana' (Youth Economic Groups).
Mbali na fedha za Serikali, kuna rasilimali fedha kwa vijana kutoka mifuko isiyo ya kiserikali na 'Programu za Wajibu wa Jamii' (Corporate Social Responsibility Programs). Ili kufikia fedha hizi, vijana wanapaswa kuunda vikundi na kujiandikisha na mamlaka za serikali za mitaa. 
Mkakati huu unalenga kuhakikisha kuwa vijana wengi wanaweza kufaidika na mzunguko wa fedha. Mwaka 2012, serikali ilianzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). 
Miongoni mwa malengo ya benki hii ni: Kuharakisha mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo,ili kuchangia ukuaji wa uchumi kwa ufanisi na endelevu pamoja na kupunguza umasikini. Benki hiyo hutoa mikopo kwa vikundi vya kiuchumi vya vijana katika kuweka mikakati ya kushiriki katika miradi ya kilimo. 
Kama msaada, benki inatoa mafunzo kwa vikundi hivyo ili waweze kutumia mikopo hiyo vizuri kwa ajili ya  kuendeleza miradi yao ya kilimo. Mpango wa TADB ni kuongezeka kwa huduma nyingine za kifedha kwa maendeleo taasisi za fedha, vyama vya ushirika, benki za biashara na taasisi ndogo ndogo za fedha ambazo zina programu za kusaidia kazi za vijana.

Umoja wa Mataifa mnami mwaka 2015 uliweka malengo 17 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu yaani SDGs ifikapo mwaka 2030 yawe yamefikiwa. Lengo namba mbili (SDGs 2) la Malengo ya Maendeleo Endelevu (Zero Hunger) linazungumzia kutokomeza njaa, kuhakikisha usalama wa chakula na lishe bora na kuendeleza kilimo endelevu ambao moja ya mkakati wa kutokomeza njaa ni kupitia kilimo ifikapo mwaka 2030. 

Ushauri kwa Vijana wa Tanzania na Afrika kwa ujumla;

Ili vijana washawishike na kuingia kwenye hii sekta ya kilimo inabidi wapatiwe mafunzo ya kilimo. Ifikapo mwaka 2050 inakadiriwa takribani watu bilioni 2.5 kutoka barani Afrika, hii ina maana gani? chakula kitahitajika kwa wingi na wakuwalisha hawa watu wote ni jitihada na nguvu za vijana wenyewe. Muda ni sasa wewe kijana unayesoma makala hii kuchangamkia fursa hii ya kilimo cha kila aina kama vile mboga mboga (horticulture), mahindi n.k. 

Hatima ya nchi yetu na bara la Afrika imebakia kwenye mikono ya vijana. Vijana ndio watu wanaoweza kuibadili Afrika isonge mbele, ni watu ambao wataibadili na kuifanya sekta ya kilimo ikue kwa kasi zaidi na ufanisi wa hali ya juu. Teknolojia imekuwa kwa kasi kila kunapokucha, imekuwa msaada kwenye sekta mbali mbali na kuimarisha ubunifu. 

Tecknolojia imeleta mapinduzi makubwa sana kwenye kilimo, hii ni pamoja na kulima kwenye eneo dogo kwa gharama nafuu na mazao yanakuwa mengi mfano mzuri ni kilimo cha 'GreenHouse' au 'Hydroponic Agriculture'. Uchumi wetu upo kwenye kilimo, afrika yetu ipo mikononi mwa vijana. Tuwamini vijana na kuwapa nafasi kwenye kilimo kwa ajili ya maendeleo endelevu na maendeleo ya nchi kufikia agenda 2063 ya Afrika tunayoitaka.  

Kupata fursa za kilimo unaweza kutembelea Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania na halmashauri yako ujipatie mkopo kupitia vikundi. 


Loading...

No comments: