Gabo Ampimia Van Vicker - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 27, 2019

Gabo Ampimia Van Vicker

Mkali wa Bongo Movie, Gabo Zigamba amefuguka kumfutalia kwa karibu staa anayetamba  Nollywood kutoka nchini Ghana, Van Vicker kwani ndiye anayemfanya ajitume sana kwenye kufanya kazi yake ya Sanaa ya uigizaji.

Akinukuliwa na gazeti la DIMBA,  Gabo aliesema wapo mastaa wengi ambao anajifunza mambo mengi kutoka kwao, lakini amekuwa akikoshwa sana na utendaji kazi wa staa huyo ambaye amedai anajifunza mengi ndani yake na hata nje ya kazi

“Kwangu Van Vicker ni msanii aliyenipa tabu sana kila nikimfuatilia, amekuwa akinifanya kuishi maisha ya kipekee sana hasa ninapotamani kuyaishi maisha yake, ananivutia ndani na nje ya sanaa yake ya kuigiza, hata maisha yake ya nje amekuwa akinifundisha vitu vingi sana, kwanza ni baba bora na amekuwa akijishughulisha na mambo mengi ya kimaendeleo,” alisema Gabo.

Gabo Zigamba ni moja kati ya wasanii wakali kutoka kiwanda cha bongo movie na mshindi wa Tuzo mbali mbali katuka tasnia ya filamu.

Loading...

No comments: