HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA LIVERPOOL, JOE GOMEZ IS BACK!!! - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 27, 2019

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA LIVERPOOL, JOE GOMEZ IS BACK!!!


Kocha wa klabu ya Liverpool mjerumani Jurgen Klopp jana amethibitisha kwamba beki wake wa kati muingereza Joe Gomez amerejea mazoezini baada ya miezi mitatu na nusu kuwa nje ya dimba. 

Klopp ameiambia tovuti ya klabu yao (Liverpoolfc.com) kuwa GOMEZ hana majeraha na anakaribia kuwa fiti 100%. 

"Amekuwa nje kwa muda mrefu,.. nafikiri Joe amekuwa nje kwa wiki 15 sasa. Huwa ni muda mrefu sana. Kwahiyo lazima aanze kutengeneza msingi upya kwa msimu huu uliobaki." 

Gomez alikuwa mbadala mzuri wa mabeki wa kati wa Liverpool pamoja na kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kabla ya kukutwa na majeraha. 
Loading...

No comments: