Haikupita siku bila Mtangazaji Ephraim Kibonde kumtaja mke wake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 9, 2019

Haikupita siku bila Mtangazaji Ephraim Kibonde kumtaja mke wake


Haikupita siku bila Mtangazaji Ephraim Kibonde kumtaja mke wake
Mtangazaji wa Clouds FM Gardner amesema kuwa ilikuwa haipiti siku bila Ephraim Kibonde kutaja jina la Mkewe wake, Sarah.

Mtangzaji Ephraim Kibonde ambaye alikuwa akishirikiana na Gardner kwenye kipindi cha Jahazi, alifariki hapo jana ikiwa ni miezi 8 tangu alipofariki mke wake.

"Nikikaaa na Kibonde huwa haipiti siku bila kumtaja mkewe na ndiyo ikafanya nigundue kuwa bado ana mawazo ya mkewe na nilikuwa nashiriki kwenye furaha yake na hata majonzi yake nikawa nashiriki baada ya kugundua hilo,” amesema Garner kwenye mahojiano na Clouds TV.

Aliendelea kwa kusema, 'Tulivyokuwa msibani kwa Boss Ruge, nilimwambia Peter Mo kuwa jukumu analolifanya Kibonde (Mc) linaweza kumrudisha kwenye mawazo na majonzi ya mkewe maana ni miezi 8 tu toka mkewe atangulie, lakini nikaambiwa kuwa yeye mwenyewe Kibonde alisisitiza kufanya mwenyewe'. 
Loading...

No comments: