Haji Manara Awakingia Kifua Wema Sepetu na Hamisa Mobetto

Msemaji wa timu Simba SC Haji Sunday Manara amewakingia kifua mastaa wa kike Wema Sepetu na Hamisa Mobetto kuwepo kwenye kamati ya kuhamasisha ushindi wa timu ya Taifa Stars dhidi ya timu ya Taifa  ya Uganda kwa kueleza sababu ya uwepo wao.Kupitia ukurasa wake kwenye mtando wa Instagram,  Manara ameandika , "wengine wanahoji hivi Kwenye kamati ya team ya Taifa, kina Wema Sepetu na Hamisa Mobetto wanafanya nini?. Hebu tuweni 'serious' kidogo guys!! . 

"Hawa wapo katika kamati ya hamasa ya timu ya taifa, na wapo watu wengi wenye ushawishiwi na kamati hii ya hamasa ipo chini yangu ikiwa chini ya kamati ya ushindi ya timu ya taifa iliyopo chini ya RC Makonda, ambapo mimi ni mjumbe. Guys hivi hamuoni hiyo kazi wanayofanya hawa wasanii na watu maarufu katika kuitangaza mechi hii ya Jumapili?. Nani leo hajui kuwa Jumapili kuna Mtanange wa kufa mtu Taifa?". Manara alimaliza.

Manara amefunguka hayo kufuatia baadhi ya watu kuhojihoji kuhusu uwepo wa wanadada hao kwenye kamati ilhali hawana uelewa wowote wa soka nchini.

Tukutane uwaja wa taifa siku ya jumapili kuishangilia timu yetu ya Taifa, Taifa Stars ikicheza na timu ya taifa ya Uganda katika kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika mwezi June, 2019 nchini Misri.

Post a Comment

0 Comments